Kuhusu sisi

Kuhusu sisi

Sisi ni nani?

Precious Present Truth, Inc. (PPT) ni shirika lisilo la faida la wainjilist walei wa kanisa la Waadventista Wasabato waliodhamiria kueneza jumbe za malaika watatu kwa Waafrika. We are preaching the Three Angels’ Messages of Revelation 14 to Africans in their native languages via media, literature, and on  ground evangelistic series. Tunaamini na kuunga mkono utume wa Jimbo Kuu la waadventista Wasabato na mpango wake wa Uhusika wa kila mmoja (Total Member Involvement) Huko Kinshasha, mwaka 2017, PPT kwa kushirikiana na jimbo konferensi mahalia ilisimamia mikutano ya hadhara iliyohudumiwa na wahubiri wa kimataifa. Mungu alizibariki juhudi zetu kwa ubatizo wa watu Zaidi ya 360.

Utume wetu:

Kushiriki kweli za Biblia na uponyaji kwa Waafrika katika lugha zao.

Kauli mbiu yetu

Hebu Jumbe za malaika watatu zifike katika ulimwengu wote ili twende nyumbani upesi

Uambukizaji

PPT inaeneza kweli za Biblia kwa kila mtu kote ulimwenguni, wale wanaozielewa lugha za Kiafrika kupitia matangazo ya televisheni, redio, tovuti yetu, program ya simu na mitandao ya kijamii.

Masomo yetu hurushwa katika televisheni na redio nchini Rwanda, Congo DRC, na Tanzania, tunatarajia kuwa na televisheni yetu ili kulifikia bara lote la Afrika.

Huduma yetu ya uinjilishaji kwa Waafrika inakua. Tunatoa huduma katika lugha sita: Kinyarwanda, Kifaransa, Kiingereza, Kiswahili, Kilingala, Kitshiluba, na tunatumaini kwamba watu wengi katika bara la Afrika watayatoa maisha yao kwa Yesu kupitia njia hizi tunazotumia kuwafikia.

Idadi ya watu ambao kwa sababu wanahudumiwa na PPT katika lugha zao ni zaidi ya milioni 283.6

HUDUMA KWA WAGONJWA NA WAHITAJI

Precious Present Truth Inc. inafuata huduma ya Kristo. Wakati Kristo akiwa duniani aliwasaidia wenye uhitaji, kwa roho hiyo hiyo, Precious Present Truth Ministry, ilianza kusaidia watoto waliodumaa (walio na utapiamlo wa kudumu) nchini Rwanda. Tunawapatia milo mitatu kwa siku kila siku (kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni) hawa watoto wenye udumavu, na wakati huo huo tunawahubiri jumbe za Marejeo kila asubuhi wanapotuleta watoto wao.

Ramani ya eneo la kufanyia kazi la PPT

Tunahudumu kikamilifu katika yafuatayo nchi:

UZALISHAJI

MIKUTANO YA HADHARA

Tunapanga kuwaalika wahubiri wazuri wa Kiadventista kutoka katika maeneo mbalimbali duniani waje kuhubiri barani Afrika, na wakati huo huo timu yetu ya mawasiliano itakuwa ikizirekodi jumbe hizi ili zirushwe katika televisheni na mitandao yetu ya kijamii.
Mungu ametubariki sana katika kazi hii kwa kuwaongoza wengi kwake, hatuna shaka kwamba ataifanikisha kwa kiasi kikubwa kuzidi tulivyofikiria.

MATOKEO

Kisa cha hivi karibuni: Watu wa Tshela, mji ulioko katikati ya Congo DRC, wamekuwa wakifuatilia jumbe hizi za malaika watatu kupitia televisheni ya Digital Congo, ambayo ni televisheni maarufu sana Congo. Neno la Mungu lilienea katika mji wote, kadri mmoja alivyomwambia mwenzake, wote wakawa na habari juu ya mahubiri haya kupitia televisheni hii. Matokeo yake, wote walishawishika na kusadikishwa kwamba wanapaswa kupumzika katika siku ya Sabato, wote walikuja kwa pamoja katika ofisi ya union ya Congo Magharibi wakiomba kujua maeneo ya karibu ambayo wanaweza kulipata kanisa la Waadventista Wasabato. Viongozi wa Union waligundua kwamba hakukuwa na kanisa huko Tshela, na kwa haraka kanisa liliwatuma walimu wa Biblia ili kuwasaidia hawa Waadventista wapya. Baada ya kufika pale, wazazi waliokuwa na watoto waliwauliza walimu hao wa biblia- Tumeshawishika kwamba tunapaswa kupumzika katika siku ya Sabato, lakini watoto wetu wanahudhuria shuleni katika siku ya Sabato, na sasa tunajua kwamba nao wanapaswa kupumzika siku ya Sabato, inawezekanaje ili nao wapumzike katika siku ya Sabato? Walimu wa Biblia waliwaomba wazazi wawajulishe idadi ya watoto hao ambao walihitaji kupumzika katika siku ya Sabato. Siku chache baadaye, wazazi walikuwa na idadi ya kustaajabisha ya wanafunzi 450. Kanisa lilifanya mpango wa kuwatafutia eneo la kufanyia ibada kila Sabato na wakaanzisha shule mpya ya Sabato katika eneo hilo kwa ajili ya watoto. Ijapokuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu, kwa sababu hawana madarasa mazuri, lakini wanamshukuru Mungu na kumheshimu katika Sabato yake.

PPT inaeneza kweli za Biblia kwa kila mtu kote ulimwenguni, wale wanaozielewa lugha za Kiafrika kupitia matangazo ya televisheni, redio, tovuti yetu, program ya simu na mitandao ya kijamii.

Masomo yetu hurushwa katika televisheni na redio nchini Rwanda, Congo DRC, na Tanzania, tunatarajia kuwa na televisheni yetu ili kulifikia bara lote la Afrika.

Huduma yetu ya uinjilishaji kwa Waafrika inakua. Tunatoa huduma katika lugha sita: Kinyarwanda, Kifaransa, Kiingereza, Kiswahili, Kilingala, Kitshiluba, na tunatumaini kwamba watu wengi katika bara la Afrika watayatoa maisha yao kwa Yesu kupitia njia hizi tunazotumia kuwafikia.

Idadi ya watu ambao kwa sababu wanahudumiwa na PPT katika lugha zao ni zaidi ya milioni 283.6

Contact Us (DRC):

Adresses:

Siège PPT ASBL Congo (DRC):
Kinshasa : Avenue Lubumbashi N1. Quartier Binza Pigeon- Commune de Ngaliema

Centre de diffusion de la Chaine PPT TV:

Goma: Rond Point Tshikudu, Boulevard Kanyamuhanga – Commune de Goma

Contact Us (Rwanda):

Adresses:

WhatsApp/Rwanda:

Watch Our Broadcast on:

Francais: DIGITAL CONGO TV via (Canal + 343)
Every Thursday 5-6h30pm (Kinshasa Time)
Every Sunday 9h40-11h10am (Kinshasa Time)

English: ISANGO STAR TV via (Canal + 386)
Every day 7-8pm (Kigali Time)
Kinyarwanda: TV1 (Canal + 383) via (Canal + 386)
Every Saturday 3-4pm (Kigali Time)
Every Sunday 2-3h30pm (Kigali Time)

This site is registered on wpml.org as a development site. Switch to a production site key to remove this banner.